Dodoma FM

Ujenzi kiwanja cha Ndege Msalato watakiwa kuongezewa kasi

17 February 2023, 12:36 pm

Ramani ya kiwanja cha Kimataifa cha Msalato Dodoma . Picha na Matukio daima Blog.

Machi 13, 2020 Tanzania na bank ya maendeleo ya afrika zilitiliana saini mkataba wa mkopo wa masharti nafuu wa Dola 495.59 milioni za Marekani (Sh1.14 trilioni) kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mitatu ya maendeleo ikiwemo uwanja wa ndege wa Msalato ambao wenyewe ulipatiwa Dola 271.63 milioni.Uwanja wa Msalato upo umbali wa kilomita 12 kutoka Dodoma Mjini barabara iendayo Arusha na ujenzi wake ukikamilika unatazamiwa kuhudumia watu 1.5 milioni kwa mwaka.

Na Fred Cheti.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule awahimiza watekelezaji wa mradi wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Msalato  wakiwemo wakandarasi wanaosimamia mradi huo kuongeza kasi ya ujenzi ili ukamilike kwa haraka.

Mh. Rosemary ameyasema hayo wakati alipotembelea katika mradi huo kuona maendeleo yake ambapo amesema ni vyema mradi huo uliofikia asilimia 11 mpaka sasa ukamilike kwa wakati kutokana na Mkoa wa Dodoma kuwa kitovu cha kupokea wageni kutoka sehemu mbalimbali Duniani kwa sasa.

Mh. Rosemary Senyamule.

Kaimu Mkurugenzi wa TANROADS Mkoa wa Dodoma Mhandisi Salehe Juma anatoa taarifa pindi mradi huo jinsi utakavyokua ukifanya kazi pindi utakapokamilika.

Mkurugenzi TANROADS