Dodoma FM

TARURA yakamilisha marekebisho ya barabara kata ya Chiboli

17 February 2023, 1:55 pm

barabara zilizo fanyiwa ukarabati . Picha na Chamwinodc.go.tz

Marekebisho hayo yanapunguza adha ya wananchi wa kata hiyo kusafiri  Umbali wa kilometa zaidi ya ishirini na nane kwa usafiri wa pikipiki.

Na Victor Chigwada                                                        

Diwani wa Kata ya Chiboli  Wiliamu Teu ameishukuru mamlaka ya usimamizi barabara za vijijini na Mijini TARURA kwa kukamilisha marekebisho kwa baadhi ya barabara ndani ya Kata hiyo

Diwani huyo Teu amesema kuwa baada ya marekebisho hayo ya TARURA imesaidia kupunguza gharama za usafiri kwa wananchi.

mh. Teu.

Aidha pamoja na marekebisho hayo bado baadhi ya vijiji vinashuhudia changamoto ya uchakavu wa miondombinu .

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kijiji cha champumba John Mdabaji  amekiri  uwepo wa barabara ndani ya kijiji hicho ambazo zinahitaji marekebisho ikiwemo ukosefu wa Makalavati

Amesema kuwa kukosekana kwa makalavati ya kupitisha maji inababisha maji kupita juu ya barabara na kusababisha changamoto ya upitaji wa magari,

John Mdabaji.