Dodoma FM

Upotevu wa wastani wa Shilingi 380,000 kwa siku umebainika

15 February 2023, 5:28 pm

Hayo ni kwa mujibu wa mkuu wa Takukuru mkoa wa Dodoma Sostheness Kibwengo ambapo amesema hiyo ni baada ya kufanya chambuzi saba za mifumo.Picha na Mwananchi

Upotevu wa wastani wa Shilingi 380,000 kwa siku umebainika katika makusanyo ya mapato ya stendi ambayo ni sawa na zaidi ya milioni 11 kwa mwezi Mkoani Dodoma .

Na Mariam Matundu.

Hayo ni kwa mujibu wa mkuu wa Takukuru mkoa wa Dodoma Sostheness Kibwengo ambapo amesema hiyo ni baada ya kufanya chambuzi saba za mifumo ya uendeshaji wa masoko ya biashara na minada na mfumo wa ukusanyaji wa mapato ya stendi .

Mkuu wa Takukuru mkoa wa Dodoma Sostheness Kibwengo.

Aidha amesema kuwa kwa kipindi cha October hadi dec 2022 Takukuru mkoa wa Dodoma imewezesha kurejeshwa kwa Zaidi ya sh milioni 200 katika miradi mbalimbali .

Mkuu wa Takukuru mkoa wa Dodoma Sostheness Kibwengo.

Bwana kibwengo ameitaja sekta ya serikali za mitaa imeongozwa kwa kulalamikiwa na wananchi mara 23 na kutoa wito kwa watendaji katika sekta za umma na binafsi kufanya kazi kwa weledi.

Mkuu wa Takukuru mkoa wa Dodoma Sostheness Kibwengo.