Dodoma FM

Kukosekana kwa elimu juu ya TASAF walengwa kutoingia kwenye mfumo

15 February 2023, 5:12 pm

Kukosekana kwa elimu ya kutosha juu ya dodoso la walengwa wa TASAF.Picha na TASAF

Imeelezwa kuwa kukosekana kwa elimu ya kutosha juu ya dodoso la walengwa wa TASAF imesababisha baadhi ya walengwa Kata ya Chilonwa kutoingia katika mfumo wa malipo.

Na Victor Chigwada.

Asheri Mkosi ni mwenyekiti wa kijiji cha Mahama amesema licha ya mradi kuendelea vizuri lakini wamekumbana na changamoto iliyotokana na dodoso lililofanywa na wasimamizi wa TASAF.

Asheri Mkosi ni mwenyekiti wa kijiji cha Mahama.

Mkosi amesema kuwa baadhi ya welengwa wamekuwa wakipata fomu za malipo zikiwa hewa kutokana na kukosea kutoa taaarifa zilizosababisha baadhi ya walengwa kushindwa kufanya kazi za mradi.

Asheri Mkosi ni mwenyekiti wa kijiji cha Mahama.

Naye Diwani wa Kata ya Chilonwa Bw.Alpha Mtuza amesema kuwa matumizi ya kidijitali ya ukusanyaji wa taarifa umechangia kuleta changamoto na kwamba hali hiyo imekuwa sio salama kwa walengwa wasio jua kusoma na kuandika .

Diwani wa Kata ya Chilonwa Bw.Alpha Mtuza.