Dodoma FM

Wakazi wa Chali Bahi kuondokana na uhaba wa huduma za Afya

13 February 2023, 1:56 pm

Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Chali Igongo wakiwa katika eneo litakapo jengwa zahanati. Picha na Benard Magawa.

Ufadhili wa ujenzi wa zahanati hiyo ni muendelezo wa ufadhili wa masuala ya afya wilayani Bahi kupitia  shirika hilo ambapo kupitia ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Bahi limefadhili huduma ya  Cliniki tembezi ya macho iliyozunguka kwenye vituo vya afya pamoja na Hospitali ya wilaya ya Bahi ambapo zaidi ya watu 477 wamefanyiwa upasuaji wa mtoto wa jicho.

Na Bernad Magawa .

Wananchi wa kijiji cha chali Igongo kata ya chali wilaya ya Bahi mkoani Dodoma wanatarajia  kuondokana na kero ya kukosekana kwa  huduma za afya kijijini hapo baada ya shirika la Qatar Charity la nchini Qatar kufadhili  ujenzi wa zahanati katika kijiji hicho.

Akizungumza katika hafla ya kumkabidhi mkandarasi wa ujenzi wa zahanati hiyo iliyofanyika wiki iliyopita   katika kijiji cha chali Igongo Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma Mbunge wa Jimbo la Bahi Keneth Nollo amesema kukamilika kwa zahanati hiyo kutafikisha Jumla ya zahanati 14  alizoshiriki kuzijenga tangu awe mbunge wa jimbo hilo miaka miwili iliyopita.

Kenneth Nollo

Diwani wa kata ya Chali ambaye pia ni makamu Mwenyekiti  wa Halmashauri ya Wilaya  Wilaya ya Bahi  Piusi Mwaluko ameeleza kuwa zahanati hiyo  itakuwa msaada mkubwa kwa  wananchi katika upatikanaji wa huduma bora za afya.

Pius Mwaluko

Kwa upande wao wananchi wa kijiji cha Chali Igongo wameeleza furaha yao kwa kusogezewa huduma kijijini kwao na kusema kuwa kilio chao cha kukosa huduma za afya kwa miaka mingi hatimaye Mungu amekisikia.

Wananchi