Dodoma FM

Bima ya Afya kwa wote itasaidia kupunguza gharama za matibabu

13 February 2023, 3:07 pm

Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma. Picha na BMH.

Muswada wa Bima ya Afya kwa Wote ambao ulikuwa uwasilishwe bungeni Wiki iliyopita ulikwama kwa mara nyingine ikiwa ni mara ya pili kwa muswada huo kukwama tangu usomwe kwa mara ya kwanza bungeni katika mkutano wa nane wa Bunge na kupelekwa katika kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kwa ajili ya kuchambuliwa.

Na Mindi Joseph.

Wananchi wamehimizwa kujiunga kwenye Bima ya afya kwa wote pindi tu Muswada wa Bima hiyo utakapopitishwa ili kuokoa gharama za matibabu.

Wananchi wengi hawana uwezo wa kumudu gharama za matibabu kama anavyozungumza Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Benjamin Mkapa Dkt.Alphonce Chandika.

Dkt. Alphonce

Naye Dkt.Angel Dillip Kutoka wizara ya afya  kuelekea katika Bima ya afya kwa wote amesema.

Dkt. Angela.