Dodoma FM

Watanzania waaswa juu ya usambazaji picha chafu mtandaoni

10 February 2023, 5:32 pm

Waziri wa habari Mh. Nape Nnauye akizungumza leo Bungeni. Picha na Bunge.

Akichangia hoja ya Mbunge wa Jimbo la Kinondoni Abbas Tarima Bungeni Jijini Dodoma ambaye aliitaka serikali kuweka mfumo maalum utakaodhibiti usambazaji wa picha chafu mitandaoni

Na Mariam Matundu.

Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya habari Nape Nnauye amewashauri watanzania kuacha kusambaza picha chafu mitandaoni .

Aidha amesema wizara yake imo katika wa kuweka mfumo maalum wa kudhibiti usambazaji wa picha chafu mitandaoni ili wananchi wasiweze kuziona Waziri Nape amesema Wizara kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA , wanauwezo mkubwa wa kubaini wahusika watakaosambaza picha chafu mitandaoni na kuwataka wananchi kuepuka kusambaza picha hizo

Waziri wa Habari