Dodoma FM

Mh.Gondwe ameagiza miradi kutekelezwa kuendana na fedha iliyotolewa na serikali

8 February 2023, 3:23 pm

Mkuu wa wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma Mheshimiwa Godwin Gondwe akiagiza miradi yote ya maendeleo wilayani.Picha na Mwananchi

Mkuu wa wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma Mheshimiwa Godwin Gondwe ameagiza miradi yote ya maendeleo wilayani humo kuanza kutekelezwa kwa wakati huku akisisitiza miradi hiyo kuendana na thamani ya fedha iliyotolewa na serikali.

Na. Benard Magawa.

Mheshiwa Gondwe ameyasema hayo alipotembelea mradi wa maji kata ya Ibihwa unaotekelezwa na Serikali ya Tanzania kupitia RUWASA wilaya ya Bahi na kusimamiwa na kampuni ya Plest Water and Civil works kwa gharama ya shilingi milioni 709 ukitarajiwa kuhudumia zaidi wananchi 7443 pindi utakapokamilika.

Mradi huo unaotarajia kuzalisha zaidi ya lita elfu 30 kwa lisaa limoja unaelezwa kuwa mkombozi kwa wananchi wa kata ya ibihwa huku wananchi na viongozi wakieleza furaha na matarajio yao huku wakiishukuru serikali ya awamu ya tano kwa mradi huo.

“Miradi yote iliyopo wilaya ya Bahi ianze kwa wakati iishe kwa wakati kwahiyo wakandarasi wote wilaya ya bahi naomba muipate hiyo ili miradi ianze kutumiwa na wanabahi, la pili lazima miradi hiyo lazima iwe sawasawa na thamani ya fedha ambayo mheshimiwa Raisi kairuhusu ije wilaya ya Bahi.”

Alisema Gondwe.

Mkuu wa wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma Mheshimiwa Godwin Gondwe .

Kwa upande wake Diwani wa katia ya Ibihwa Mheshimiwa Mwijuki Benjamini ameahidi kushirikiana kikamilifu na mkandarasi ili mradi uweze kukamilika kwa wakati huku akiahidi kusimamia maagizo yote yaliyotolewa na Mkuu wa wilaya.

Mheshimiwa Mwijuki Benjamini.