Dodoma FM

Wafanyabiashara walalamikia hali ya soko Ihumwa

7 February 2023, 12:39 pm

Hali ya soko la Ihumwa jijini Dodoma.Picha na Martha Mgaya

Wafanyabiashara katika soko la ihumwa jijini dodoma wameiomba serikali kutengeneza miundombinu ya soko hilo kutokana na eneo wanalotumia kwa sasa kutokutosheleza mahitaji.

Na Thadei Tesha.

Ni katika soko la ihumwa jijini dodoma ambapo baadhi ya wafanyabiashara katika soko hili wanasema halitoshelezi mahitaji yao.

Wananchi na wafanya biashara wakilalamika.

Bi Rehema Ibrahimu yeye pamoja na kuwa ni mfanyabiashara katika soko hilo lakini pia ni mwenyekiti wa soko la ihumwa hapa anaeleza ni kwa namna gani wanaathirika na changamoto hiyo na juhudi za kuboresha soko hilo.

Mwenyekiti Bi Rehema Ibrahimu.

Pamoja na kuwa soko hilo linasaidia wakazi wa mtaa wa ihumwa ukosefu wa vyoo, udogo wa soko na udogo wa stendi ya daladala ni miongoni mwa changamoto ndani ya soko hilo.