Dodoma FM

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Ataka Ujenzi ukamilike

3 February 2023, 11:39 am

Mkuu wa mkoa akizungumza na wasimamizi wa ujenzi wa kituo cha Afya cha Itiso.Picha na Martha Mgaya

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh. Rosemary Senyamule amewataka wasimamizi wa ujenzi wa kituo cha Afya cha Itiso kilichopo wilayani Chamwino kuharakisha ukamilishaji wa ujenzi wa kituo hicho ili kianze kutoa huduma kwa wananchi.

Na Fred Cheti

Mkuu huyo wa Mkoa ametoa maagizo hayo alipofanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani humo ambapo.

“ameonesha kutofurahishwa na mwenendo wa ujenzi wa kituo hicho cha afya ambacho kinagharimu zaidi ya shilingi milioni 500.”

Mkuu wa mkoa Mh. Rosemary Senyamule.
Mganga mkuu akiongelea hatua iliyofikia ya ujenzi huo.Picha na Martha Mgaya

Venance Mgaiga ni Kaimu Mganga Mkuu wa halmshauri ya wilaya ya Chamwino anaeleza hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa kituo hicho na nini kinakwamisha mpaka sasa mradi huo kutokukamilika.

Venance Mgaiga Mganga mkuu.
Mkuu wa wilaya ya Chamwino Gift Msuya.Picha na Martha Mgaya

Mkuu wa wilaya ya Chamwino Gift Msuya amesema kumekuwa na mvutano wa pande mbili kati ya ujenzi wa kituo hicho na uongozi wa kata jambo ambalo linachangia kuchelewesha kukamilika kwa mradi huo.

Gift Msuya.