Dodoma FM

TARURA kutatua changamoto ya barabara Chamwino

2 February 2023, 10:46 am

Baadhi ya barabara zilizo chini ya Tarura. picha na Tarura

Wakala wa barabara vijiji na mijini Tarura inatarajia kutatua changamoto ya barabara wilayani Chamwino kupitia bajeti ya mwaka 2023/2024.

Na Seleman Kodima.

Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Chamwino imesema inatarajia kutatau changamoto ya Miundombinu ya Barabara  katika wilaya ya Chamwino kwa asilimia 200  kupitia bajeti  ya mwaka 2023/24 ambayo  itagharimu bilion 4.48  .

Akizungumza na Taswira ya Habari Meneja wa TARURA wilaya ya Chamwino Mhandisi Nelson Maganga amesema Bajeti hiyo itaongezeka ikiwa ni sambamba na ahadi ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na fedha nyingine.

Amesema Fedha hizo zimegawanyika katika makundi matatu ,ambapo zipo fedha za matengenezo kiasi cha Shilingi billioni 1 milion 489 .

Mhandisi Nelson Mganga.