Dodoma FM

Wananchi Bahi watakiwa kupanda miti ili kulinda vyanzo vya maji

31 January 2023, 12:02 pm

Aina ya kitalu cha miti. picha na Mwananchi

Wananchi wilayani Bahi wametakiwa kuboresha mazingira na kutunza vyanzo vya maji kwa kuhakikisha wanapanda miti kwa wingi na kuilinda ili kutunza mazingira na vyanzo vya maji.

Na Bernad Magawa

Wito umetolewa kwa wananchi  Wilayani Bahi kupanda miti kwa wingi na kuepukana na ukataji holela wa miti kwaajili ya mkaa ili waweze kuimarisha uhifadhi wa mazingira na kulinda vyanzo vya maji.

Wito huo umetolewa na Ofisi ya Uhifadhi wa misitu TFS ya Bahi na kuwahimiza wananchi kuacha mazoea ya kukata miti ovyo ili kuepukana na madhara ya mabadiliko ya tabia nchi.

Akizungumza Mhifadhi misitu wilaya ya Bahi Byela Kahangwa alipokuwa akizungumza na mwandishi wa Dodoma fm ofisini kwake amesema.

Akielezea kuhusuana na tatizo la uchomaji holela wa mkaa wa kupikia amesema tatizo hili ni kubwa walayani hapo kiasi cha kusababisha madhara makubwa kwa mazingira ambayo ni muhimu kwa maisha ya mwanadamu na viumbe vingine.

Amesema uhifadhi wa misitu husaidia kulinda vyanzo vya maji na kusaidia upatikanaji wa mvua za kutosha hivyo misitu inapoharibiwa maisha ya mwanadamu yanakuwa hatarini.

Amewasisitiza wanachi wilayani humo kupanda miti ya kutosha na kufuata utaratibu wa kukata miti ili kutokuharibu mazingira kwa kukata miti ovyo jambo ambalo linahatarisha ustawi wa viumbe hai.