Dodoma FM

Bodaboda Bahi walalamika kuto nufaika na stendi

23 January 2023, 11:25 am

Na; Bernad Magawa .

Madereva wa bodaboda wilayani Bahi Mkoani Dodoma wameelezea kutokunufaika na stendi ya mabasi wilayani humo .

Hayo yamesema na Mwenyekiti wa madereva wa boda boda Wilaya ya Bahi Bw Mohamedi Mongoya mapema leo wakati akizungumza na taswira ya habari wilayani humo ambapo amesema kuna baadhi ya taratibu zime wekwa na wilaya hiyo  hazina usimamizi mzuri.

Amesema hapo mwanzoni mabasi yote ya mikoani na daladala walipaswa kushushia abiria ndani ya stendi lakini kwa sasa usimamizi wa taratibu hizo umelegalega hivyo abiria wameanza kushushwa na kupakiwa eneo lolote jambo ambalo linawapa wakati mgumu waendesha bodaboda katika kupata wateja.

Amesema uongozi wa wilaya hiyo ulipoketi nao katika kikao uliwaelekeza kuwa stendi hiyo itakuwa fursa kwa waendesha boda boda kwa kujiongezea kipato lakini kwa sasa hali imebadilika hivyo kuiomba serikali kusimamia kikamilifu sheria walizoziweka ili nao waweze kunufaika.

Akizungumzia kuhusu malalamiko hayo Diwani wa kata ya Bahi Agostino Ndonu amesema  sheria na taratibu zote zilizowekwa na Halmashauri bado zipo pale pale na kuwaasa madereva wote kufuata sheria na taratibu zilizowekwa na wilaya.

Kituo cha Mabasi   ya Bahi kilianzishwa na Serikali wilayani humo ikiwa na lengo la kupanua na kukuza mji wa bahi huku boda boda wakitarajiwa kuwa miongoni mwa wanufaika wa stendi hiyo kwa kusafirisha abiria kutoka mji wa bahi .