Dodoma FM

Wiki ya Sheria yazinduliwa Jijini Dodoma

22 January 2023, 10:59 am

Na; Fred Cheti.

Makamu wa Rais wa Jamhuriya muungano wa Tanzania dkt. Philp Mpango amesema uchumi endelevu wa wananchi utafanikiwa iwapo vyombo vya utoaji haki vitatimiza wajibu wake katika kusikiliza na kutoa haki kwa wananchi bila upendeleo wowote.

Dkt. Mpango ametoa kauli hiyo waakati akihutubia katika uzinduzi wa wiki ya sheria nchini, shughuli iliyofanyika katika viwanja vya nyerere square jijini Dodoma

Amesema kaulimbiu ya maadhimisho ya wiki ya sheria mwaka huu imelenga kuchochea uchumi wa wananchi jambo ambalo linaweza kufanikiwa iwapo swala la utoaji haki kwa wananchi litatekelezwa bila uonevu wowote.

Makamu wa rais amesema ni wajibu wa kila mwananchi kushirikiana na mahakama kutatua migogoro kwa njia ya usuluhishi ili kusaidia kupunguza mrundikano wa kesi mahakamani.

Jaji mkuu wa Tanzania prof. Ibrahim Hamis Juma amesema kupitia wiki ya sheria majengo manne ya mahakama za wilaya maeneo mbalimbali nchini ili kusogeza huduma za mahakama karibu na wananchi.

Kilele cha maadhimisho ya wiki ya sheria kitakuwa February 1 mwaka huu katika viwanja vya chinangali park jijini dodoma ambapo mgeni rasmi atakuwa rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.