Dodoma FM

Wananchi watakiwa kuacha ubinafsi

18 January 2023, 2:20 pm

Na; Lucy Lister.

Naibu waziri wa sanaa utamaduni na michezo na mbunge wa jimbo la Babati mjini Mh. Pauline Gekul amewataka watanzania kuacha ubinafsi na kuwa na moyo wa kusaidia wengine kama alivyofanya baba wa Taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa kutenga maeneo ya wapigania uhuru kwa nchi za Afrika

Gekul ameyasema hayo wilayani Kongwa alipokuwa katika ziara yake ya kutembelea maeneo yenye historia ya ukombozi wa nchi za Afrika katika mikoa ya Dodoma na Morogoro ili kujionea hali ya uhifadhi wa maeneo hayo

Sambamba na hayo Gekul amesema wizara yake itaongeza bajeti kwaajili ya maeneo hayo kwani ni kivutio na sehemu ya muhimu kwa historia ya taifa na mataifa mengi ya Afrika kama Angola, Zimbabwe, Afrika Kusini, Namibia na Msumbiji

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Kongwa mh Remidius Mwema amesema historia ya maeneo ya wapigania uhuru yanaipatia nchi heshima kubwa kimataifa na kueleza hatua walizochukua kama wilaya kuhifadhi maeneo hayo.