Dodoma FM

Waganga wa tiba asili waomba mafunzo kutoka wizara ya Afya

13 January 2023, 3:56 pm

Na; Mariam Matundu.

Waganga wa tiba asili nchini wameiomba wizara ya afya kuwezesha waganga kote nchini kupata mafunzo ya namna bora ya kufanya kazi zao yatakayosaidia kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa .

Akizungumza mwenyekiti wa umoja wa waganga wa tiba asili Bujukana John amesema iwapo waganga wote watapata mafunzo na kuboresha dawa zao zitasaidia pia kupata masoko ya kimataifa.

clip 1 mwenyekiti……………

Mmoja wa waganga hao amesema kuwa ni wakati sasa wa kupambana na matapeli ,wanaopa nafas ya uganga kwani imekuwa ikiathiri kazi zao na kujenga chuki kati yao na wananchi .

clip 2 mganga ………………….

Nae maneja maabara kutoka ofisi ya mkemia mkuu wa serikali John Faustin amesema wameamua kutoa mafunzo kwa waganga wa tiba asili ili kuwapa mafunzo na kuwataka waganga kutoa ushirikiano ili kutoa matibabu bora kutokana na dawa zao.

clip  ofisi ya mkemia………………..

Hata hivyo ofisi ya mkemia mkuu imewakutanisha waganga 400 wa tiba asili kuwapa mafunzo ya namna bora na salama ya kusindika na kujenjua dawa za asili.