Dodoma FM

Elimu ya chanjo ya uviko 19 ni muhimu kwa wazazi

12 January 2023, 1:59 pm

Na; Mariam Matundu.

Imeelezwa kuwa ni muhimu kwa wazazi na walezi kupata chanjo ya uviko 19 kwani mbali na kujilinda wao wenyewe lakini pia husaidia kuwalinda watoto.

Bi Lotalisi Gadau  ni mratibu wa mpango wa taifa wa chanjo kutoka wizara ya afya amesema kuwa endapo watu wengi watapa chanjo hiyo wanaweza kuwakinga  watoto wadogo kwani wapo ambao hawawezi  kupata chanjo hiyo ya uviko 19.

Aidha ametaja madhara yanayoweza kumpa mtoto iwapo wazazi au walezi wasipopata chanjo ya uviko 19.

.

Hata hivyo amesema kwa sasa muamko wa wananchi kupata chanjo za uviko 19 umeongezeka tofauti na mwanzoni na kusisitiza kuwa chanjo hizo ni salama na zinatolewa bure.

.

Taswira ya habari imepita mtaani na kuzungumza na wazazi na walezi kutaka kujua iwapo wanafahamu kuwa ukipata chanjo ya uviko 19 unaweza kumlinda mtoto?

Chanjo ya uviko 19 inapatikana katika vituo vya afya kote nchi bila malipo ambapo hutolewa kwa watu wenye umri kuanzia miaka 18.