Dodoma FM

Chamwino wajadili mustakabali wa utunzaji Mazingira

11 January 2023, 2:14 pm

Na; Mariam Kasawa.

Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Pamoja na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Chamwino jana amekutana na Wadau wa Mazingira, watendaji wa Kata, Viongozi wa Taasisi za Umma na Wahe. Madiwani kwa ajili ya kujadili masuala mbali mbali yanayohusu mustakabali wa utunzaji wa mazingira wilayani humo.

Majadiliano hayo yalijadiliwa kuhusu, uondoshaji wa taka pamoja na mazoezi ya upandaji wa miti na muhimu zaidi uandaaji wa Vitalu vya miti kwa kila Kata.

Aidha ametumia kikao hicho kutoa maelekezo ya Viongozi wa Kitaifa juu ya masuala yahusuyo mazingira, ikiwemo maelekezo ya Mkuu wa Mkoa  kuwa kila kaya ipande miti 5 na Maelekezo ya Ofisi ya Makamu wa Rais  mazingira juu ya utunzaji wa vyanzo vya maji, usafi wa mazingira na upandaji wa miti.

.