Dodoma FM

Wakazi wa Silwa walalamika kukosa huduma ya Umeme

1 December 2022, 8:11 am

Na; Victor Chigwada . 

Pamoja na jitihada za kusambaza umeme zinazo endelea nchini katika maeneo yaliyopo nje ya miji lakini bado baadhi ya maeneo yameendelea kuwa na kilio cha huduma hiyo.

Wakizungumza na taswira ya habari baadhi ya wananchi wa kijiji cha Silwa wamedai huduma hiyo kukatiza katika maeneo yao na kuelekezwa kwenye baadhi ya taasisi

.

Mwenyekiti wa kijiji hicho Bw.Zakalia Masinjisa amekiri licha ya kuwepo kwa umeme katika taasisi za elimu na mali ya sili lakini changamoto kubwa imekuwa ni kukosekana kwa huduma hiyo kwa wananchi

Hata hivyo ameishukuru Serikali kwa jitihada za Serikali kwa kuhakikisha taasisi za elimu zinafikiwa na huduma ya umeme itakayo saidia wanafunzi kwa masomo ya ziada na kujisome

.

Naye Diwani wa Kata ya Pandambili Bw. Onesmo Nywage amesema kuwa umeme upo katika vijiji vyote kwa awamu ya kwanza

Amesema kuwa endapo zoezi la umeme jazilizi litawafikia watakuwa mefanikisha huduma hiyokwa wananchi wa kata yake

.

Kusambaa kwa huduma ya umeme nchini kunaweza kuleta chachu ya ujenzi wa viwanda viodogovidogo amabvyo vitapunguza wimbi la ukosefu wa ajira