Dodoma FM

Serikali yasaini mkataba wa uzalishaji na ugawanaji mapato

1 December 2022, 7:29 am

Na; Mariam Kasawa.

Baada ya miaka 12 Serikali ya Tanzania imesaini mkataba wa uzalishaji na ugawanaji mapato (PSA) kitalu cha RUVUMA – MTWARA.

Mkataba huu unaweka utaratibu wa serikali kupata zaidi. Kwa mara ya kwanza Serikali inapata kwenye Mapato ghafi (Gross) ambapo Kwenye huu mkataba serikali inapata 75%, ukilinganisha na huko nyuma ambapo ilikua inapata 68% kushuka chini.

Waziri wa Nishati, Januari Makamba akiwa kwenye utiaji saini mkataba wa uzalishaji na ugawanaji mapato (PSA) kitalu cha Ruvuma – Mtwara, Waziri Makamba amesema sasa nchi inaanza kuingia kwenye uchumi wa gesi.

.

Amesema mlolongo wa matukio na jitihada za Serikali.  Kule Arusha,wapo  kwenye hatua za mwisho za majadiliano kwenye mradi  wa kuchakata gesi utakao gharimu zaidi ya trilioni 70 ambao  utakuwa uwekezaji mkubwa barani Afrika.

.