Dodoma FM

Bahi sokoni waiomba serikali kuongeza madara

1 December 2022, 7:16 am

Na; Benard Filbert.

Wananchi wa wilaya ya Bahi Kata ya Bahi Sokoni wameiomba serikali kuongeza madarasa shule ya Msingi Bahi Sokoni ili kukidhi idadi ya wanafunzi waliopo katika shule hiyo.

Wakizungumza na taswira yahabari wamesema ni vyema serikali ika ongeza madarasa kwani wanafunzi waliopo katika shule hiyo ni wengi ikiringanishwa na madarasa yaliyopo.

Kwa upande mwingine wamesema athari zinazojitokeza ni baadhi ya wanafunzi kushindwa kujifunza vizuri katika masomo yao.

.

Agustino Ndunuu ni Diwani wa kata ya Bahi sokoni amekiri kuwepo kwa wanafunzi wengi katika shule ya msingi Bahi Sokoni lakini amesema mpango uliopo hivi sasa ni kujenga shule mpya na tayari maandalizi ya kujenga shule hiyo yamekamilika.

.

Hata hivyo amesema wamekuwa wakijitahidi kuanzisha shule nyingi za msingi katika kata hiyo ili kukidhi mahitaji ya wanafunzi kutokana na ongezeko la watoto mara baada ya sense ya watu na makazi iliyofanyika hivi karbuni.