Dodoma FM

Wanafunzi watakiwa kuepuka hofu

16 November 2022, 12:36 pm

Na; Lucy Lister.

Hofu inayowakumba baadhi wanafunzi kipindi cha mitihani imetajwa kuwa ni moja ya sababu inayofanya wanafunzi wengi kufeli na wengine kukatisha masomo yao.

Wakizungumza na taswira ya habari baadhi ya walimu mkoani Dodoma wamesema kuwa hofu inaweza kumsababishia mwanafunzi kushindwa kuendelea na mtihani hivyo kuzimia kwenye chumba cha mtihani na wakati mwingine hupelekea kifo.

Adelina Defonsi ni mwalimu wa hesabu ameeleza kuwa maandalizi ya mtihani kwa mwanafunzi yasipokuwa mazuri yanamfanya kupata matatizo kama kuzimia na wakati mwingine kumsababishia kufeli mtihani.

Nae mtaalamu wa Saikolojia kutoka shirika la KISEDEK liliyopo Chamwino amesema kuwa matatizo ya kuanguka kwa wanafunzi kipindi cha mitihani yanatokana na msongo wa mawazo

Pia ametoa ushauri kwa wanafunzi kufanya maandalizi kwa kujua jukumu lao na kuwekeza muda mwingi katika kusoma,na kumwomba Mungu  ufahamu katika masomo.