Dodoma FM

Rais Samia kutangaza matokeo ya awali ya sensa 0ct 31 Jijini Dodoma

27 October 2022, 10:08 am

Na; Mariam Matundu.

Imeelezwa kuwa maandalizi ya uzinduzi wa matokeo ya mwanzo ya sensa ya watu na makazi yamefikia hatua nzuri hivyo wananchi wametakiwa kujitokeza kwa wingi kushuhudia matokeo hayo yakitangazwa.

Hayo yameelezwa na mkuu wa mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule wakati akizungumza katika kipindi cha the morning power show na kusema kuwa Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan atatangaza matokeo hayo jijini Dodoma hivyo ni muhimu wakazi wa Dodoma kuitumia fursa hiyo kwa kufika uwanjani .

.

Aidha amesema kuwa maandalizi hayo yamezingatia huduma zote za kijamii ikiwa ni pamoja na kuyaangalia makundi maalumu ya watu wenye ulemavu pamoja na wazee.

.

Nae mtakwimu kutoka ofisi ya taifa ya takwimu NBS Mariam Kitembe amesema matokeo yatakayotangazwa siku hiyo ni yale yanayohusu idadi ya watu kwa nchi nzima .

.

Mkoa wa Dodoma umepewa heshima ya kutangaza matokea ya mwanzo ya sensa ya watu na makazi iliyoanza agost 23 na kukamilika sep 5 ambapo matokeo hayo yanatarajiwa kutangazwa oct 31 katika uwanja wa jamuhuri na mh Rais Samia Suluhu Hassani.