Dodoma FM

Wakazi wa Chenene waiomba serikali iwafikishie huduma ya umeme

21 October 2022, 9:57 am

Na; Benard Filbert.

Wakazi wa kijiji Cha Chenene wilaya ya Chamwino wameiomba serikali kuwafikishia huduma ya  nishati ya umeme ili kusaidia uchumi wa kijiji hicho kukua zaidi.

Hayo yamesemwa na wakazi wa kijiji hicho wakati wakizungumza na taswira ya habari kuhusu hali ya huduma ya  umeme ilivyo hivyo sasa.

Wamesema kuna nguzo ambazo zilihifadhiwa katika kijiji cha chenene na baadaye zikachukuliwa kupeleka kijiji cha jirani hali iliyozua taharuki kwani baadhi yao waliamini nguzo hizo ni kwa ajili ya kijiji cha Chenene.

.

Baadhi ya wanawake wamesema kitendo cha kukosa umeme katika kijiji hicho inasababisha  kutembea umbali mrefu kutafuta mashine kwa ajili ya kusaga nafaka.

.

Taswira ya habari inaendelea kuwatafuta viongozi wa eneo hilo ili kujua mkakati walio nao katika kutatua changamoto ambayo imekuwa ikiwakabili wananchi.