Dodoma FM

Ukosefu wa wahudumu wa Afya katika Zahanati ya Chunyu wapelekea huduma hafifu

21 October 2022, 10:42 am

Na;Mindi Joseph.

Ukosefu wa Wahudumu wa afya katika zahanati ya Chunyu wilayani Mpwapwa imetajwa kuwa changamoto  inayowakabilia  wananchi  pindi waendapo kupata huduma nyakati za Usiku

Akizungumza na Taswira ya habari Mwenyekiti wa Kijiji hicho Bw Abineli Masila amesema zahanati hiyo inawahudumu wawili tu jambo ambalo ni kikwazo kwa wananchi katika kupata huduma nyakati zote.

Ameiomba serikali kusaidia kupatikana kwa wahudumu wengine wa afya ili kutatua changamoto hiyo.

.

Kwa upande wa wananchi wa kijiji hicho wamesema Zahanati hiyo haikidhi mahitaji yao.

.

June Mwaka huu serikali ilitangaza kuwapangiwa vituo vya kazi wahudumu wa afya  6,876 Huku maeneo mengi ya Vijiji yakiendelea kukabiliwa na uchache wa wahudumu wa afya.