Dodoma FM

Wakazi jijini Dodoma waomba kupunguziwa gharama za usafirishaji

18 October 2022, 6:44 am

Na; Mariam Matundu. 

Wananchi jijini  Dodoma wameomba kuboreshewa usafirishaji ili kupunguza gharama za usafiri zinachochangia kupanda kwa gharama za maisha siku hadi siku.

Denis mandia ni mkazi wa dodoma yeye amesema kuwa suala la kupanda kwa gharama za usafirishaji zinachochea umasikini miongoni mwa watu kwa kuwa bidhaa zinapanda bei mara dufu.

.

Kwa upande wake Devota Mwakyoma mkazi wa Dodoma amesema pamoja na hayo lakini serikali imeweka mipango mathubuti ya kuwakomboa vijana ,wanawake na watu wenye ulemavu kwa kuweka mikopo isiyo na riba.

.

Taswira ya habari imezungumza na mchambuzi wa masuala ya kijamii Bwana Ismail Mussa ambapo amesema sera ya taifa ya maendeleo kwa vijana  imesaidia kwa kiasi kikubwa kuimarisha uchumi kwa wananchi .

.

kwa  mujibu wa tafiti za mapato na matumizi uliofanywa na ofisi ya taifa ya takwimu kwa kusirikiana ya kimataifa ikiwemo bank ya dunia umasikini umepungua kutoka 39%mwaka 1991/92 hadi kufikia 26.4%mwaka 2018