Dodoma FM

Wasichana wataka usawa katika ugawaji wa majukumu

12 October 2022, 11:59 am

Na; Mariam Matundu.

Usawa katika  ugawaji wa majukumu ya nyumbani kwa wasichana ni mzigo ambao umekuwa ukiwalemewa .

Siku ya mtoto wakike Duniani yenye kaulimbiu isemayo Haki zetu ni hatma yetu ,wakati ni sasa ,Baadhi ya wasichana wamesema suala la majukumu ya kazi za nyumbani imekuwa ni kikwazo kwa wanafunzi wakike na kuwasababishia kukosa muda wa ziada wa kusoma ukilinganisha na wanafunzi wakiume.

.

Aidha wameomba wadau kujitokeza kusaidia kujenga mabweni katika shule zilizopo mbali ,kwani itasaidia kushinda vikwanzo wanavyokutana navyo njia kwakuwa baadhi wanalazimika kutembea umbali mrefu.

.

Taswira ya habari imezungumza na mwalimu wa shule ya msingi Soya Johari Juma  pamoja na mwalimu wa shule ya sekondari kwa Mtoro Agnes Rwesya  ambapo wamesema kuwa wamekuwa wakiwapa elimu ya kujitambua wasichana ili watimize ndoto zao .

.

Katika kuhakikisha huduma za malezi ikiwemo malezi kwa wasichana zinaboreshwa ,serikali kupitia wizara ya maendeleo ya jamii jinsia wanawake na makundi maalumu imetoa mafunzo ya malezi chanja kwa wazazi na walezi kwa lengo la kuwezesha makuzi bora katika halmashauri 132 ambapo vikundi vya malezi 1,184 vimeanzishwa katika mikoa 17 ya Tanzania bara hadi kufikia jun mwaka huu 2022.