Dodoma FM

Uhaba wa madarasa Miganga wawanyima uhuru wanafunzi

12 October 2022, 12:43 pm

Na; Benard Filbert.

Uhaba wa madarasa katika shule ya msingi Miganga kata ya Idifu wilaya ya Chamwino imetajwa kuwa kikwazo cha wanafunzi kujifunza kwa uhuru.

Hayo yameelezwa na wazazi wa wanafunzi katika kijiji cha Miganga wakati wakizungumza na Taswira ya habari ambapo  wamesema madarasa ni yaliyopo hayakidhia hali ya wanafunzi waliopo kutokana na uchache wake

Wameiomba serikali kufanya ukarabati wa madarasa hayo ili wanafunzi waweze kujisomea pasipo bugudha.

.

Taswira ya habari imeungumza na mwenyekiti  wa Kijiji Cha Miganga John Mawaya ambapo amekiri kuwepo kwa changamoto ya madarasa hali ambayo sio kawaida.

Ametaja idadi ya wanafunzi waliopo katika shule hiyo amesema hadi sasa kuna wanafunzi zaidi ya 1000 na  madarasa yakiwa  ni saba pekee huku baadhi ya wanafunzi wakisoma katika eneo ambalo ni jiko la shule

.

Uhaba wa Madarasa imekuwa changamoto kubwa hususani shule za vijijini huku serikali ikitakiwa kutatua changamoto hiyo ili kuwasaidia wanafunzi kujifunza bila vikwazo.