Dodoma FM

Wananchi watakiwa kuchukua tahadhari dhidi ya Ebola

4 October 2022, 12:41 pm

Na;Mariam Matundu.

Wakazi wa Dodoma wametakiwa kuendelea kuchukua tahadhari ya ugonjwa wa ebola  kwa kuepuka kula nyama pori ambazo hazija kaguliwa na wataalamu , kuepuka mikusanyiko pamoja na kuzingatia suala la unawaji mikono mara kwa mara.

Tahadhari hiyo imetolewa Dkt Gasper Kisenga kutoka ofisi ya Mganga mkuu Dodoma Jiji  ambapo amesema licha ya ugonjwa wa ebola kutoingia nchini  lakini ni muhimu  wananchi kuchukua tahadhari.

.

Amezitaja baadhi ya dalili za ugonjwa wa ebola kuwa ni pamoja na kutokwa na damu katika sehemu za mwili zilizowazi ,kuumwa mafua ,kupata maumivu mwilini na kusisitiza kuwa ni muhimu kuwahi hospitali pindi utakapoona dalili hizo.

.

Taswira ya habari imezungumza na baadhi ya Wananchi  ambapo wamesema bado elimu haijawafikia ipasavyo na kuomba wataalamu wa afya kuongeza juhudi ya utoaji wa Elimu kwa Umma.

.

Itakumbukwa kuwa ugonjwa wa ebola umeripotiwa nchini uganda ambapo pia vifo kadhaa vimeripotiwa huku wizara ya afya nchini Tanzania imetangaza kuchukua tahadhari juu ya Ugonjwa huo.