Dodoma FM

Sheria ndogo ndogo zapelekea wananchi kujenga vyoo bora Chemba

4 October 2022, 12:25 pm

Na; Benard Filbert.

Uwepo wa Sheria ndogo ndogo  katika Halmashauri ya wilaya ya chemba umetajwa kusaidia wananchi kujenga vyoo bora

Katika kutekeleza na kusimamizi  sheria hizo ,wenyeviti wa vijiji wamepewa jukumu la kuhakikisha wananchi katika vijiji vyao wanajenga vyoo bora.

Kijiji cha kwa mtoro ni miongoni mwa vijiji vinavyotambulika katika halmashauri ya wilaya ya chemba  wakiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ujenzi wa vyoo bora kwa wananachi wake

Hussein Bakari Chande  ni mwenyekiti wa kijiji hicho anaeleza namna ambavyo amehakikisha sheria hiyo inasimamiwa katika kijiji chake.

.

Aidha Mwenyekiti huyo anaeleza namna ambavyo usimamizi wa sheria hiyo umeweza kuzaa matunda kwa wananchi na kusababisha muitikio wa ujenzi wa vyoo bora

.

Taswira ya habari imezungumza na baadhi ya wananchi katika kijiji cha kwa mtoro kujua namna ambavyo wameitikia agizo la serikali kujenga vyoo bora katika makazi yao.

.

Mwaka 2020 serikali kupitia mkurugenzi wa kinga kutoka wizara ya afya DKT. Leonard Subi wakati akitoa tamko la siku ya choo duniani alitangaza kuwepo kwa ongezeko la kaya zenye vyoo bora kutoka asilimia 59 mwaka 2019 hadi kufikia asilimia 63.7 june mwaka 2020