Dodoma FM

Kata ya mnadani yaipongeza Dodoma fm Radio .

16 September 2022, 1:57 pm

Na; Benard Filbert.

Mwenyekiti wa mtaa wa Karume kata ya Mnadani Jijini Dodoma Bw Matwiga Kiatya ameipongeza Dodoma Fm kwa kuripoti habari kuhusu changamoto ya barabara katika mtaa huo ambayo kwa sasa ipo kwenye mchakato wa Ujenzi

Akizungumza na taswira ya habari kuhusu marekebisho ya barabara za ndani Katika mtaa wa Karume,Matwiga Amesema kuwa kupitia Dodoma Fm wananchi walikuwa wakitoa kero zao kuhusu barabara za mtaa huo hali ambayo imesababisha viongozi kusikia kero hizo na kufanyia kazi.

.

Kabla ya marekebisho hayo Bwana Matwiga amesema barabara zilikuwa hazipitiki kirahisi kutokana na ubovu.

.

Baadhi ya wananchi wa mtaa wa Karume wakizungumza na taswira ya habari wamepongeza jitihada za Dodoma Fm huku wakiitaka serikali kuendelea kuboresha zaidi barabara hizo.

Miundombinu ya Barabara katika mtaa wa karume Kata ya Mnadani ilikuwa ni kikwazo kwa wakazi wa eneo hilo  katika ukuaji wa maendelea katika nyanja za kiuchumi