Dodoma FM

Umbali wa shule wapelekea baadhi ya wanafunzi Pandambili kuacha shule

1 September 2022, 9:30 am

Na; Victor Chigwada.

Umbali mrefu wanaotembea wanafunzi wa sekondari  lenjulu  mpaka pandambili umetajwa kuwa kikwazo cha kuwakatisha tamaa na kushindwa kumaliza masomo.

Hilo limefahamika baada ya Taswira ya Habari kuzungumza na baadhi ya Wananchi ambapo Wamesema kuwa adha hiyo ya umbali mrefu  inaweza sababisha baadhi ya wanafunzi kujihusisha na vitu hatarishi ambavyo vinaweza kukatisha ndoto za masomo yao

.

Mwenyekiti wa Kijiji Cha Lenjuli Bw.Enock Mahungo ameeleza jitihada ambazo wamezichukua kutatua changamoto hiyo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa vyumba vya madarasa

.

Naye Diwani wa kata ya Lenjulu  Bw.Brown Chisondela amekiri kukabiliwa na changamoto hiyo ya kutokukamilika kwa vyumba vya madarasa ya sekondari Jambo linalowapa mtihani kwani wanatarajia kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza kwa mwezi January 2023

.