Dodoma FM

TRC kuimarisha ulinzi na usalama wa mizigo kwenye Treni

10 August 2022, 2:04 pm

Na;Mindi Joseph .

Shirika la Reli Tanzania limesema limejipanga kuhakikisha linaimarisha ulinzi na usalama wa mizigo ya abiria kwenye Treni kwa  kudhibiti vitendo vya wizi vinavyofanyika.

Hayo yamebainishwa na Mkurungezi Mkuu TRC Masanja Kadogosa kufuatia changamoto hiyo ambayo imekuwa ikijitokeza na amekiri kuwa kuna wizi umekuwa ukifanyika kwa watu kuingilia dirishani na kuiba mali na mizigo ya abiria.

Ameongeza kuwa treni zote zitakuwa na Cctv kwa ajili ya ulinzi na Madirisha yote hayatafunguliwa wakati wa safari kama ilivyo kwa sasa.

.

Katika hatua nyingine amegusia changamoto ya kutokuwepo kwa Mtandao katika baadhi ya maeneo na kusema miundombinu ya mitandao kwa sasa imerahisishwa hata maeneo ya porini .

.