Dodoma FM

Wazazi watakiwa kutoa taarifa za vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa watoto wao

29 July 2022, 1:34 pm

Na; Benard Filbert.

Wazazi wametakiwa kushirikiana na kutoa taarifa pindi wanapoona vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa watoto wao ili kuepusha athari wanazoweza kukutana nazo watoto hao.

Hayo yanajiri kutokana na kukithiri kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia katika jamii licha ya serikali kupitia vyombo vya sheria ikiwepo dawati la jinsia kuwekeza jitihada kudhibiti vitendo hivyo.

Baadhi ya wazazi wakizungumza na taswira ya habari wamesema mzazi yeyote anao wajibu wa kutoa taarifa pindi anapoona sintofahamu kwa mtoto na kutoa taarifa katika sehemu husika ili kudhibiti ukatili kwa watoto.

.

Daniel Sande ni mwanasheria kutoka Shirika la haki yangu Tanzania ameiambia taswira ya habari kuwa taasisi hiyo imeanzisha kampeni ya TWAWEZA ambayo imelenga kutoa elimu katika shule za msingi nchini katika masuala ya ukatili wa kijinsia.

Kadhalika amesema elimu hiyo imelenga kuwafungua wananchi kutoa taarifa pindi wanaposhuhudia hali hiyo.

.

Ili kuzuia vitendo vya kikatili jamii inaaswa kutoa taarifa katika vyombo vya sheria ili kushirikiana kwa pamoja kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa watoto.