Dodoma FM

Ripoti mbalimbali za taasisi ya wajibu kutumika Bungeni ili kuleta uwazi

20 July 2022, 1:37 pm

Na;Mindi Joseph.     

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya bajeti Mh Daniel Sillo amesema kuwa wataendelea kutumia ripoti mbalimbali za taasisi ya wajibu bungeni katika kuleta uwazi na uwajibikaji.

Akizungumza na Taswira ya habari amesema ripoti hizo nne za taasisi ya wajibu kwa mwaka 2020/21 zimekuwa na matokeo chanya kutokana na namna zilivyorahishwa uchambuzi wake ili  kuyafikia makundi mbalimbali ya watu.

.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi taasisi ya wajibu Yona Killagame amesema kuwa ripoti za mwaka huu zipo nne huku kukiwa na maboresho mengi katika ripoti hizo.

.

Nao baadhi ya wakazi Mkoani hapa wamesema kuwa uchambuzi huu unaofanywa na taasisi ya wajibu  ni msaada katika kufahamu juu ya matumizi ya fedha za serikali.

.