Dodoma FM

Mkoa wa Dodoma kuanza mkakati mpya wa kilimo cha Alizeti

19 July 2022, 11:14 am

Na; Benard Filbert.

Serikali ya mkoa wa Dodoma kwa kushirikiana na wizara ya viwanda na biashara inatarajia kuanza mkakati mpya wa kilimo cha alizeti ili kuhamasisha watu kujihusisha na kilimo hicho kwa wingi.

Hayo yameelezwa na mkuu wa mkoa wa Dodoma Bwana Antony Mtaka wakati akizungumza na taswira ya habari kuhusu mkakati wa mkoa juu ya zao la alizeti.

Amesema kuwa serikali ya mkoa inatamani kuwa na kilimo cha alizeti ambacho kinavutia wawekezaji kwa kuzingatia kilimo cha kisasa ambacho kitaleta hamasa kwa vijana.

.

Bwana Mtaka amesema kwa kushirikiana na wizara ya viwanda na biashara wamepata ekari 500 katika wilaya ya Kongwa pamoja na wawekezaji kutoka shirika la world Food Program WFP ambao watafunga mashine za kusindika alizeti.

.

Baadhi ya wakazi wamesema mkakati huo ni mzuri endapo utafanikiwa hivyo ni vyema ukawahusisha wakulima wa zao hilo ili wahamasike.

Dodoma ni miongoni mwa mkoa ambao unazalisha zao la alizeti kwa wingi pamoja na mafuta ya zao hilo huku mikoa mingi ikitegemea mafuta ya alizeti kutoka kanda ya kati.