Dodoma FM

Wanaume wakwepa kushiriki suala la uzazi wa mpango

4 July 2022, 1:30 pm

Na;Mindi Joseph.    

Imeelezwa kuwa wanaume wengi si washiriki wazuri katika suala la uzazi wa mpango hatua inayosababisha wanawake wanaoamini uzazi wa mpango kuamua kutumia njia za usiri na hivyo kukosekana maridhiano baina ya pande hizo.

Akizungumza leo na Taswira ya habari Elizabeth Mwai Muuguzi Kutoka kituo cha afya makole amesema baadhi ya wanawake wamekuwa wakitaka kushiriki uzazi wa mpango, lakini, kutokana na kuwahofia waume zao, wamejikuta wakipata huduma hiyo kwa kujificha.

.

Ameongeza kuwa jamii bado ina imani potofu kuhusu dhana nzima ya uzazi wa mpangohali inayopelekea wanawake wengi kutojitokeza kutumia uzazi wa mapango.

.

Uzazi wa mpango unatoa uhueni  kwa familia  katika kuwatunza  watoto hao pamoja na kuwapatia huduma nzuri, kwa vile panakuwepo na maandalizi ya kiuchumi kabla ya kupokelewa mtoto mpya.