Dodoma FM

Hali ngumu ya maisha yachangia uharibifu wa mazingira

29 June 2022, 2:34 pm

Na; Victor Chigwada.

Hali ngumu ya maisha imetajwa kuwa  sababu ya watu kuendelea kuharibu mazingira ikiwa Ni pamoja na ukataji wa misitu ovyo hususani maeneo ya milimani na vijijini

Diwani wa Kata ya Chipanga Bw.Masumbuko Aloyce amekiri kuwa changamoto kubwa ya uharibufu wa  mazingira imechagizwa na matumizi ya jamii kutokana na mahitaji yao ya kimaisha

Amesema kuwa watu wengi Wanao jihusisha na ukataji miti wamekuwa na malengo ya kuanzisha mashamba mapya na wengine kudai kutumia Kama matumizi ya mkaa majumbani

.

Aloyce ameiomba Serikali kusaidia kupeleka wataalamu wa kuwaelimisha wananchi juu ya utunzaji wa mazingira ambayo itapunguza Kasi ya uharibifu wa misitu hiyo