Dodoma FM

TANESCO yazindua huduma ya NIKONECT

23 June 2022, 2:18 pm

Na; Benard Filbert.

Shirika la umeme nchini Tanesco limezindua huduma ya kuwaunganishia umeme wananchi kwa haraka inayofahamika kama NIKONEKT  ambayo inafanyika mtandaoni pasipo kwenda kwenye ofisi za shirika hilo.

Hayo yameelezwa na Sarah Libogoma afisa uhusiano na huduma kwa watejaTanesco Mkoa wa Dodoma wakati akizungumza na taswira ya habari kuhusu huduma hiyo.

Amesema huduma ya NIKONECT imekuja wakati sahihi ambapo itarahisisha foleni katika ofisi mbalimbali za shirika hilo na mwananchi atapata huduma akiwa nyumbani.

Kadhalika amesema kwa atakaye tumia huduma hiyo ataunganishiwa umeme ndani ya siku chache kutokana na kuimarika kwa mfumo huo.

.

Katika hatua nyingine amewataka wananchi kuzingatia matumizi salama ya umeme ili uwasaidie katika shughuli za kiuchumi na si vinginevyo.

.

Huduma ya NIKONECT ambayo imezinduliwa na shirika la umeme tanesco nchini itasaidia kuhudumia wateja washirika hilo kwa haraka na kuepusha mlundikano wa watu ambao umekuwa ukitokea katika ofisi za shirika hilo.