Dodoma FM

Taasisi yajiwekea lengo la kutokomeza vitendo vya rushwa kwa asilimia 80

10 June 2022, 3:40 pm

Na; Benard Filbert.

Taasisi ya SAUTI YA WAPINGA RUSHWA inayojihusisha na kutoa elimu dhidi ya vitendo vya rushwa nchini imeweka lengo la kutokomeza vitendo hivyo hadi kufika asilimia 80 itakapofika mwaka 2024.

Hayo yameelezwa na  Bwana Haruna Kitenge mwenyekiti wa mabalozi wa taasisi hiyo wakati akifanya mahojiano na taswira ya habari kuhusu malengo ya taasisi hiyo katika kuzuia na kupambana na rushwa.

Amesema katika kuhakikisha wanafikisha elimu hiyo ya kukomesha vitendo vya rushwa nchini wamekuwa wakitoa elimu hiyo kupitia makundi mbalimbali ya vijana huku wakiamini elimu itafika kwa haraka.

.

Hata hivyo amesema hivi sasa wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii kufikisha elimu hiyo ili kuhakikisha wanamfikia kila mmoaja.

Kadhalika amesema kuwa hivi karibuni wanatarajia kuanza kutekeleza kampeni yao mpya SEPESHA RUSHWA ambayo itawafikiwa watu wengi wakiwepo madereva bodaboda.

.

Taasisi ya SAUTI YA WAPINGA RUSHWA yenye makao yake makuu jijini Dar Es Salaam imejikita katika kuelimisha jamii kupambana na vitendo vya rushwa aina zote kwani rushwa ni adui wa haki.