Dodoma FM

Sejeli yaiomba serikali kusaidi ujenzi wa vyumba vya madarasa

10 June 2022, 3:56 pm

Na; Victor Chigwada.

Wananchi wa kijiji cha Mbande Kata ya Sejeli Wilaya ya Kongwa wameiomba Serikali kuwasaidia ujenzi wa vyumba vya madarasa kutokana na idadi kubwa ya wanafunzi kwa sasa

Baadhi ya wananchi hao wakizungumza na Taswira ya habari wamesema vyumba vya madarasa vimelemewa na idadi ya wanafunzi licha ya ujenzi wa shule nyingine kwa nguvu za wananchi kukwama kifedha

.

Mwenyekiti wa kijiji cha Mbande Bw.Peter Ekiyumbe ameeleza idadi kubwa ya wanafunzi imetokana na ukuaji wa kijiji chao hivyo kupelekea hitaji la vyumba vingine vya madarasa

.

Naye Diwani wa Kata hiyo Bw.Chilingo Chimeredia amesema kuwa kutokana na idadi kubwa ya watoto katika shule ya msingi Mbande  wameamua kuanzisha ujenzi wa shule nyingine kwa nguvu za wananchi

.

Serikali imekuwa na utaratibu wa kuunga mkono juhudi za wananchi katika kutatua changamoto zinazo wakabili