Dodoma FM

Serikali yaendelea kukemea uharibifu wa mazingira

9 June 2022, 3:41 pm

Na ;Victor Chigwada.

Pamoja na wimbi la uharibifu wa mazingira unao kua kwa kasi kutokana na matumizi ya nishati ya mkaa na kuni Serikali umeendelea kukemea suala hili ili kulinda uoto wa asili

Mwenyekiti wa Kijiji Cha Kazania Bw.Mganga Kuhoga amekiri kuendelea kuwachukulia hatua stahiki watu Wanao shiriki vitendo vya ukataji miti ovyo kwa kuwafikisha mahakamani

.

Naye Diwani wa Kata ya Ngh’ambi Bw.Richadi Milimo amesema kuwa jitihada za kupambana na wakaidi wa uharibifu wa mazingira kwa kuwafuatilia kwa karibu kwa nyakati zote hususani muda wa usiku ambao huutumia kufanya uharibifu

.

Ukataji miti ovyo unaweza kupelekea mmomonyoko wa udongo na hata kusababisha ukame kwa kukosa mvua za kutosha