Dodoma FM

Serikali kufanya uwekezaji wa lishe kupambana na utapia mlo

9 June 2022, 3:32 pm

Na;Mindi Joseph Chanzo.

Serikali imeahidi kufanya Uwekezaji Kitaifa katika lishe nchini kama sehemu ya mapambano dhidi ya utapiamlo kuanzia ngazi ya Kaya hadi Taifa.

Akizungumza Jijini Dodoma Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu  (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. George Simbachawene katika kikao kazi  cha Watendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania pamoja na wadau wa maendeleo amesema hii inalenga kuhakikisha jamii inakuwa salama na kushiriki katika shughuli za uzalishaji.

Mhe. Simbachawene amesema kama Taifa ni muhimu kuweka jitihada za pamoja katika mapambano hayo kwani ukosefu wa lishe umekuwa na madhara makubwa kwa watanzania  na kushindwa kufanya shughuli za uzalishaji kwa ufanisi.

.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania Dkt. Germana Leyna amesema wataendelea kushirikiana na serikali, kushauri, kuongoza na kuhamasisha lishe .

.

Aidha ipo haja ya elimu ya lishe kufundishwa katika shule za msingi kuanzia darasa la kwanza hadi la saba ili kuwandaa vijana kuwa mabalozi  wazuri wa lishe katika maeneo  yao.