Dodoma FM

Nishati mbadala itaepusha uharibifu wa mazingira

8 June 2022, 3:10 pm

Na; Benard Filbert.

Jamii imeshauriwa kutumia nishati mbadala hali itakayosaidia kuepuka uharibifu wa mazingira hivyo kuchangia mabdailiko ya tabia ya nchi.

Ushauri huo umetolewa na meneja wa mamlaka ya hali ya hewa kanda ya kati bwana Isdory Kilenga wakati akizungumza na taswira ya habari kuhusu mwenendo wa mabadiliko ya hali ya hewa nchini.

Bwana Isdory amesema kuwa ili kuepuka mabadiliko ya tabia ya nchi ni vyema jamii ikahamia kwenye matumizi ya nishati mbadala kama gesi.

.

Kadhalika ameishauri jamii kuacha kuishi kwa mazoea na badala yake watafute taarifa rasmi za mabadiliko ya hali ya hewa ili waendane na nyakati husika.

.

Akizungumzia kuhusu hali ya baridi iliyopo hivi sasa amesema ni kutokana na jua kuwa mbali ya uso wa dunia pamoja na kukithiri kwa upepo ikitofautishwa na vipindi vingine.

.

Mamlaka ya hali ya hewa inawajibu wa kutoa taarifa za mabadiliko ya hali ya hewa ili wananchi na mamlaka zingine waweze kuchukua tahadhari kutokana na mabadiliko hayo kwa maslahi ya nchi.