Dodoma FM

Uhifadhi wa milima ya Tao umesema utaendelea kuhakikisha maeneo yanayo zunguka hifadhi hiyo yanatunzwa

1 June 2022, 2:50 pm

Na;Mindi Joseph. 

Katika kuendelea kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi Mfuko wa uhifadhi wa milima ya Tao la mashariki umesema utaendelea kuhakikisha mimea,wanyama na vyanzo vya maji  katika maeneo ya Hifadhi vinatunzwa.

Akizungumza katika mahojiano na Dodoma Fm Afisa Miradi Kanda ya kusini Rosemary Boniphance kutoka Mfuko wa uhifadhi wa milima ya Tao la mashariki amesema wamejikita katika upande wa hifadhi kwani maeneo hayo yanasaidia kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

.

Ameongeza kuwa Hadi sasa kupitia Mfuko huo miradi ya jamii wamefanikiwa kufikia halimashauri 12 ambazo zipo katika hifadhi 9.

.

Kwa upande wake Jophillene Benjumula afisa mahusiano na utafutaji wa Rasilimali Mfuko wa uhifadhi wa milima ya Tao la mashariki amesema wanafanya jitihada mbalimbali za kuhifadhi misitu na kuinua jamii inayozunguka misitu hiyo.

.

Nao Baadhi ya wananchi wanaozunguka Hifadhi ambapo mradi huu unatekelezwa wameushukuru mfuko huo kwani umewasaidia kujikwamua kiuchumi na kulinda misitu hiyo.

.

Mfuko wa uhifadhi wa milima ya Tao la mashariki unafanya kazi katika hifadhi 9 na unashirikiana na wadau mbalimbali ili kuendeleza shughuli za uhifadhi wa mistu katika milima na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.