Dodoma FM

Ujenzi wa vyumba vya madarasa waendelea Bahi

30 May 2022, 4:34 pm

Na;Mindi Joseph.   

Ujenzi wa madarasa katika shule za sekondari na Msingi kata ya bahi unaendelea ili kuhakikisha wanatatua changamoto ya Madarasa kwa wanafunzi.

Akizungumza na Taswira ya habari Diwani wa kata hiyo Bw,Agustino Ndonuu amesema wananchi wameunganisha nguvu kwenye jitihada za serikali ili kuhakikisha madarasa hayo yanakamilika kwa wakati.

Ameongeza kuwa serikali iliwapatia fedha kwa ajili ya ujenzi wa madarasa hayo.

.

Aidha amesema kwa upande wa shule za msingi madarasa 4 yameshakamilika.

.

Katika hatua nyingine amepongeza taasisi zisizo za kiserikali kwa kuendelea kusaidia katika ujenzi wa miundombinu ya elimu.