Dodoma FM

Uharibifu wa misitu wailetea nchi hasara ya asilimia 5%ya pato la Taifa

27 May 2022, 2:45 pm

Na;Mindi Joseph.  

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Selemani Jafo amesema takriban hekta laki nne ( 469,420) za misitu huharibiwa kila mwaka Nchini.

Akizungumza leo jijini Dodoma na Waandishi wa Habari Waziri Jafo amesema hali hii inaathiri maisha ya viumbe mbalimbali ikiwemo ya mifumo ikolojia ambapo  hadi sasa imeliletea Taifa hasara ya takriban asilimia tano (5%) ya Pato la Taifa.

Ameongeza kuwa utupaji holela wa taka pamoja na uwepo wa athari za mabadiliko ya tabianchi yamekuwa ni changamoto kubwa katika nchi

.

Aidha ametoa wito kwa Mikoa yote nchini kuhamasishana na kuelimisha jamii masuala yahusuyo hifadhi ya mazingira ikiwemo kutumia nishati mbadala wa mkaa na majiko banifu.

.

Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani Kitaifa mwaka huu yatafanyika katika Jiji la Dodoma na kaulimbiu ya kitaifa  ni ”Tanzania ni moja tu: Tutunze Mazingira”na Kilele kitatanguliwa na Wiki ya Mazingira inayoanza  kesho mei 28 hadi  4 Juni ambapo shughuli mbalimbali za hifadhi na usafi wa mazingira zitafanyika katika maeneo mbalimbali zikuhusisha wananchi, taasisi, mashule, vyuo na viongozi mbalimbali.