Dodoma FM

Jamii yatakiwa kutofumbia macho ajali zinazo athiri macho

27 May 2022, 2:58 pm

Na;Yussuph Hassan.    

Jamii imeshauriwa kutofumbia macho ajali mbalimbali zinazoathiri macho kwani kufanya hivyo ni kuhatarisha uoni ambao unaweza kusababisha upofu baadae.

Ushauri huo umetolewa na Bingwa wa Magonjwa ya Macho kutoka kliniki ya Cvt Dodoma Dkt Nelson Mtajwaa wakati akizungumza na kituo hiki ambapo amesema mashambulizi mbalimbali ya jicho huweza kusababisha madhara ya uoni.

.

Aidha amesema kwa kawaida magonjwa ya macho ni nadra mtu kufahamu pasi na kufanyiwa uchunguzi, hivyo ni vyema jamii ikajenga utamaduni wa kupima afya ya macho mara kwa mara ikiwemo presha ya macho.

.

Kadhalika baadhi ya wakazi mkoani Dodoma wameomba serikali iendelee kutoa elimu juu magonjwa ya macho kutokana  na dodoma kuwepo na ugonjwa huo kutokana na mazingira yake.