Dodoma FM

Halmashauri zatakiwa kutenga maeneo maalum kwaajili ya shughuli za ubunifu

19 May 2022, 3:29 pm

Na;Yussuph Hassan.

Wito umetolewa kwa halmashauri Nchini kutenga maeneo maalum kwa ajili ya shughuli za kukuza bunifu zinazofanywa na wabunifu mbalimbali.

Wito huo umetolewa na makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Philip Mpango katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya bunifu Jijini Dodoma ambapo amesema kufanya hivyo kutasaidia kuibua bunifu nyingi zaidi.

.

Naye Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali imejipanga kikamilifu kukuza wabunifu nchini huku akizitaka taasisi zinazowasaidia wabunifu kutoa elimu juu ya hakimiliki za bunifu zao.

.

Aidha kwa upande wake Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia Prof Adolf Mkenda amesema mashindano hayo ni mara nne kufanyika huku makundi ya washiriki kwa mwaka huu yakiwa ni saba.

.

Kilele cha Wiki ya bunifu imeenda sambamba na utoaji wa zawadi kwa washindi wa bunifu mbalimbali nchini na kuhudhuriwa na viongozi wa kiserikali na taasisi mbalimbali.