Dodoma FM

Wazazi / walezi jijini Dodoma watakiwa kuwapeleka watoto kupata chanjo ya polio

18 May 2022, 2:19 pm

Na;Mindi Joseph.

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amesema ugonjwa wa polio hauna tiba na unasababisha madhara kiafya ikiwemo kupooza kwa viungo vya mwili.

Akizungumza leo jijini Dodoma katika uzinduzi wa kampeni ya kitaifa ya chanjo ya matone dhidi ya ugonjwa wa polio kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano amesema ugonjwa huu unaambukizwa na huathiri watu wa rika zote na hauna tiba.

Amesema takwimu zinaonyesha unaathiri zaidi watoto ambapo kuanzia mwaka 1975 Tanzania ilianza kutoa chanjo ya kuwakinga watoto dhidi ya ugonjwa wa polio..

.

Isaa Ibrahimu amezaliwa mwaka 1993 na alikuwa mgonjwa wa kwanza Nchini tanzania kupata ugonjwa wa polio Mwaka 1996 amesema anashindwa kutekeleza majukumu yake kikamilifu.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mh Antony Mtaka amewataka wazazi kushriki katika zoezi hili ili kuwakinga watoto wao na ugonjwa wa kupooza wa polio.

.

Kauli mbiu ya kampeni ya kitaifa ya chanjo ya matone dhidi ya ugonjwa wa polio kwa watoto wa umri chini ya miaka mitano ni Kila tone la chanjo ya polio litaiweka Tanzania salama dhidi ya ugonjwa wa kupooza.